Numbers 12:6-8

6 aBwana akasema, “Sikilizeni maneno yangu:

“Akiwapo nabii wa Bwana miongoni mwenu,
nitajifunua kwake kwa maono,
nitanena naye katika ndoto.
7 bLakini sivyo kwa mtumishi wangu Mose;
yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote.
8 cKwake nitanena naye uso kwa uso,
waziwazi wala si kwa mafumbo;
yeye ataona umbo la Bwana.
Kwa nini basi ninyi hamkuogopa
kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Mose?”
Copyright information for SwhNEN